Majukumu ya Wizara
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ina Majukumu yafuatayo:
- Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera za Sekta ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
- Kuendeleza, kuwezesha na kuratibu masuala ya kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara.
- Kusimamia Vyombo vya Habari (Magazeti na vituo vya Redio na Televisheni).
- Kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Michezo nchini.
- Kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Utamaduni nchini.
- Kusimamia utendaji wa Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala, Miradi na programu zilizo chini ya Wizara.