Habari

Imewekwa:: Oct, 04 2019
News Images

.Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ametoa kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma kushiriki katika Bonanza la Michezo.

Bw.Singo ametoa wito huo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya bonanza hilo litakaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi Oktoba 5, 2019.

Akiendelea kuzungumzakatika mkutano huo Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa kama ilivyo desturi ya wizara hutekeleza uhamasishaji wa mazoezi ya viungo kwa vitendo kama ilivyoagizwa na Mheshimiwa Mkamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

‘’Bonanza hili litakuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo mazoezi ya viungo,mbio za polepole (Jogging), Mchezo wa Kuvuta Kamba pamoja na Mpira wa Miguu,’’alisema Bw.Singo.

Pamoja na hayo Bw.Singo alisistiza kama ilivyokawaida wizara inapoandaa bonanza linakuwa kubwa lenye shamra shamra nyingi na mpaka sasa wizara zote na taasisi zote za serikali zimekwisha alikwa kushiriki bonanza hilo.

Kwa upande wa mwalimu wa mazoezi atakayeongoza zoezi la mazoezi ya viungo Bw.Simba Said kutoka Home Fitness Centre Dodoma alisema kuwa yuko vizuri na amejiaanda vyema kutoamzoezi yatakayo boresha afya kwa watu wote watakaohudhuria hivyo wakazi wa Dodoma wajitokeze kwa wingi.