News

Posted On:: Oct, 13 2021
News Images

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Machifu na Viongozi wa Kimila ni kiungo muhimu kwa Serikali katika kudumisha amani, na maendeleo ya taifa.

Dkt. Abbasi Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha kupokea maoni kutoka kwa Machifu, kuhusu uhuishaji wa Sera ya Utamaduni Oktoba 5, 2021 Ukumbi wa African Dreams jijini Dodoma

Kikao hiki kinafuatia maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika Tamasha la Utamaduni lilioandaliwa na Umoja wa Machifu Tanzania (MUT) Septemba 8, 2021 jijini Mwanza.

Rais Samia aliitaka Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo iwashirikishe Machifu katika kuhuisha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997.

Zaidi ya Machifu na Viongozi wa Kimila 105 kutoka mikoa yote nchini.

Dkt. Abbasi amewataka Machifu kuunga mkono juhudi za Serikali na kuleta maendeleo kwa taifa.

Amesema tayari Serikali imeshaanzisha Mfuko wa Sanaa na Utamaduni kwa ajili ya kuboresha utamaduni wetu ambao umetengewa shilingi bilioni 1.5

Naye Makamu Mwenyekiti wa (UMT) ambaye pia ni Chifu wa Unyanyembe Tabora Chifu Msagata Fundikila ameipongeza Serikali kwa kuwashirikisha Machifu katika kikao hicho.

Amesema kikao hiki kimekuja katika wakati mwafaka kwa kuwa utamaduni wa taifa umekuwa ukiharibiwa an utandawazi.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emanuel Temu amesema Serikali imeamua kuhuisha Sera ya Utamaduni kutokana na kuathiriwa na tamaduni za kigeni

Amesisitiza kuwa Sera inahuishwa ili iende na wakati na kanuni na Sera nyingine kama Sera ya Malikale na Elimu