News

Posted On:: Mar, 01 2021
News Images

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesisitiza somo la Historia kufundishwa shuleni na utunzaji wa historia na utamaduni wa nchi.

Mhe.Bashungwa ameyasema hayo Februari 27, 2021 alipomuwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika kufunga wiki ya Mashujaa wa Majimaji Mjini Songea Mkoa wa Ruvuma ambapo alisisitiza kuhifadhiwa kwa maeneo ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.

"Nawashukuru wananchi wa Ruvuma kwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza na kuhifadhi kumbukumbu ya historia ya nchi yetu maana mkoa huu ulikuwa kambi adhimu kwa wapigania uhuru wa Msumbiji"alisema Mhe.Waziri.

Aidha Mhe.Bashungwa alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kurudisha somo la Historia kwenye shule zote nchini, huku akiupongeza uongozi wa manispaa ya Songea kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo kufundisha somo hilo.

Pia Mhe. Waziri Bashungwa ameendelea kupongeza Serikali kwa kuendelea kupigia chapuo lugha ya kuswahili kama ambavyo Mhe. Rais Dkt. Magufuli alivyoagiza na kutekeleza matumizi ya Kiswahili katika uendeshaji wa shughuli za kesi mbalimbali nchini.

Katika ziara hiyo Mhe. Bashungwa aliongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Songea Mjijini Dkt. Damas Ndumbaro, pamoja na Chifu wa Wangoni Emmanuel Zulu Gamma na kuelez kuwa Serikali inafanya jitihada ya kufungamanisha Utalii na Utamaduni wa nchi.

Sherehe hizo zimefanyika ikiwa ni kukumbuku ya vita ya Majimaji ambapo mashujaa Zaidi ya 60 akiwepo mmoja mwanake Bi Mkomanile wanakumbukwa kwa namna walivyojitoa katika harakati za kutafuta uhuru wa watu wa Ruvuma