News

Posted On:: Mar, 25 2021
News Images

Katika uhai wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alikipigania alipigania Sekta ya Sanaa katika kuhakikisha haki na maslah ya wasanii yanalindwa na kuheshimiwa.

Akizungumza na wanahabari Machi 24, Wilayani Chato Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi ameeleza kuwa Katika kampeni zake za mwaka 2015 aliahidi kuinua sekta hii na alitekeleza vyema kwa kuwa Rais wa kwanza kuunda wizara yenye sekta ya sanaa inayojitegemea, huku akieleza kuwa katika ahadi zake mwaka 2020 akitilia mkazo zaidi namna ya kuinua zaidi sekta hiyo.

"Leo hatuko naye mtu huyu Dkt. John Pombe Magufuli, bingwa katika kuipigania sekta ya sanaa, anapaswa kuimbiwa, nyimbo za maombolezo, nyimbo za kumwombea pumziko la amani na la milele."Hivyo Machi 25 (leo) kuanzia saa 10 kamili jioni hadi saa moja katika uwanja wa Magufuli hapa Chato tumewapa nafasi wasanii wote watakaoweza kufika Chato na waliokwishafika Chato kumuimbia Magufuli kwa nyimbo mbalimbali za maombolezo walizozitunga mmoja mmoja na kama makundi," alisema Dkt. Hasaan Abbasi,

Dkt. Abbasi alieeleza kuwa Wasanii Zaidi ya 40 wametunga nyimbo za maombolezo na watapewa nafasi ya kuomboleza kupitia nyimbo hizo wilayani Chato katika kushiriki shughuli mbalimbali za kumuaga Magufuli.

"Serikali imeridhia ratiba hii ya wasanii kupata nafasi ya kumuaga kiongozi wao lakini pili baadaye kumwimbia katika tukio maalum litakalokuwa mbashara katika redio na TV mbalimbali nchini. Hii ni heshima kubwa kwa wasanii na ni heshima kubwa kwa Mzee wetu Dr. Magufuli," alisema Dkt. Abbasi.