Habari

Imewekwa:: Aug, 26 2019
News Images

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa waandaji wa mashindano ya michezo mbalimbali kufika maeneo ya vijijini kusaka wachezaji kwakua maeneo hayo yana vijana wengi wenye vipaji.

Mhe.Mwakyembe amesema hayo jana Wilayani Mbulu wakati akifunga michuano ya mpira wa miguu ilioandaliwa na Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe.Flatei Maasai yaliyoitwa FlateiCup 2019 ambapo ameeleza kuwa michezo katika dunia ya leo ni ajira hivyo vijana waliopo vijijini wanapaswa kushiriki mashindano mbalimbali ili kuonesha vipaji walivyonavyo.

“Michezo sio afya tu, wala burudani pia ni ajira rasmi katika ulimwengu wa leo, hivyo ni vyemawaandaji wa mashindano mbalimbali ya michezo kufika maeneo ya vijijini kusaidia wenye vipaji waweze kuonekana” alisemamhe.Mwakyembe.

Kwa upande wake muandaaji wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe.Flatei Maasai amesema kuwa lengo la kuandaa mashindano hayo ni kusaidia vijana kuonyesha vipaji walivyonavyo ili waweze kupata ajira pamoja na kuongeza kipato chao.

Aidha Mhe.Flatei ameipoongeza Serikali kwa kuongeza juhudi za kuimarisha sekta ya michezo nchini kwakua ni Sekta ambayo inajiri vijana wengi na ambayo inasaidia kuimarisha afya za wananchi.

Mashindano hayo ya jimbo la Mbulu Vijijini yameshirikisha timu mbalimbali ambapo timu iliyoshinda ni Maretadu FC ambayo imekabidhiwa kombe na zawadi ya fedha.

….