Habari

Imewekwa:: Aug, 03 2020
News Images

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza rasmikuwa kuanzia Julai 29, 2020 Uwanja wa Taifa uliopo Jijini Dar es Salaam umebadilishwa jina nakuitwa Uwanja wa Benjamin William Mkapa ili kumuenzi Rais huyo wa awamu ya Tatu aliyeagadunia usiku wa kuamkia Julai 23, 2020.

Rais Magufuli ametoa tamko hilo, Julai 29, 2020 katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwarais wa Serikali ya Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Uwanjawa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa Mzee Mkapa alikuwa namchango katika sekta ya michezo nchini hivyo taifa linapaswa kumuenzi .

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo na alikua hapendi vitu viitwe kwa jinalake,lakini kwa vile sasa amelala na hawezi kuniadhibu na kwakua nimepokea ujumbekutoka watu wengi wakiniomba nibadili jina la uwanja wa Taifa, nimekubali na sasanatamka rasmi kuwa uwanja huu uitwe Mkapa Stadium,” alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa Mzee Mkapa ni kiongozialiyekuwa anapenda michezomichezo na amefanya mambo mengi katika sekta hiyo,vile vile alikua ni shabiki wa timu yaYanga ingawa hakuwahi kuonyesha hadharani hivyo watanzania wanatakiwakumkumbuka na kutunza kumbukumbu hizo.

Halikadhalika, Rais Magufuli aliongeza kuwa Mzee Mkapa ndiye muanzilishi waChama cha Hakimiliki na Hakishiriki(COSOTA)ambayo ni taasisi yenyelengo la kuwasaidia wasanii kupata haki za kazi zao nakatika Sekta ya Habari, alianzisha Vitengo vya Habari na Mawasiliano Serikalini.

Naye, shabiki wa mpira nchini Bw.Athuman Ugassa amepongeza uamuziwa Rais Magufuli kubadilisha jina la Uwanja wa Taifa na kuuita Uwanja wa Mkapakwani uwanja huo ni alama ya mchango wa Mzee Mkapa katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.