News

Posted On:: Mar, 18 2021
News Images

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa ameeleza azma ya Serikali kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika kuhakikisha kazi za wasanii wa pande zote mbili zinanufaisha wasanii wote pindi kazi hizo zinapouzwa kwenye minada.

Mhe.Bashungwa ameeleza hayo Machi 17, 2021 katika mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania na Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti ambapo wamekubaliana kushirikiana katika sekta za wizara yake.

Aidha, Mhe Waziri amesema Serikali itaendelea kushirikana na Umoja huo kupitia Taasisi ya Hakimili Tanzania (COSOTA) ili kuleta tija katika masuala ya ubunifu hasa muziki na kuongeza kipato kwa wasanii na wadau wengine wenye haki katika bunifu mbalimbali.

Mhe.Waziri Bashungwa amesisitiza pia ushirikiano na Umoja huo katika Taasisi za COSOTA, TaSUBa na Chuo cha Michezo Malya.