Habari

Imewekwa:: Mar, 20 2020
News Images

Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amwaahidi ushirikiano msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu Chid benz.

Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipofanya kikao na msanii huyo ambapo Chid benz alimuhakikishia kuwa kwa sasaamebadilika na anataka kuwaonyesha watanzania amefanikiwa kujikwamua katika matumizi ya madawa ya kulevya na hataki tena kurudi huko kwani anazaidi ya miezi mitatu sasa hajatumia madawa hayo kabisa.

“Kati ya wasanii wenye kukubalikana mashabiki zao wewe Chid benzni mmoja wao na mashabiki zako ni wengi hivyo ningependa kukuona kwanzia sasa unalijenga zaidi jina lako kwa kuonyesha kuwa umebadilika,katika kipindi hichi nitafurahi zaidi kukuona unasonga mbele na hurudi tena katika matumizi ya madawa ya kulevya wizara ipo pamojana wewe kukusaidia wakati wowote ,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho mheshimiwa Shonza alimsisitiza msanii huyo kuwaonyesha watanzania kuwa anaweza na hata akipewa nafasi anaweza kujitumia vyemana kuonyesha juhudi yake katika kufanya kazi na kuwa mbunifu katika kufanya kazi zake za usanii.

Naye Msanii huyo wa Bongofleva Chid benz alieleza kuwa kwa sasa hautarudi nyuma tena sababu tayari amekwisha acha kutumiamatumizi ya madawa hayo na ninaelewa bahati haiji mara mbili lakini kwangu naiona imekuja zaidi ya mara moja kwa maana ya kuwa nimekuwa nimekuwa na anguka nainuka narudi kwa mashabiki wananipokea nakuendelea kukubali muziki wangu hakika najiona niwakati wa kuwafurahisha zaidi mashabiki na sitawaangusha.

“Ombi langu kwa serikali ni kupata ushirikiano na mapema wiki ijayo ninatarajia kutoa wimbo wangu mmoja uitwao Beautiful ambao nimeuiamba nikisifu uzuri wa mwanamke na kufuatia janga la Corona ninamwahidi mheshimiwa Naibu Waziri kuwa nitatunga wimbo kwa ajili ya Corona ,”Chid benz.

Pamoja na hayo nae Chid benz alitoa wito kwa watanzania kuacha kufanya mzaha katika mitandao ya jamii kuhusu suala la ugongwa Corona sababu hili ni tatizo ni janga linalosumbua dunia kwa sasa hivyo jambo la msingi ni kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali kutoka kwa wataalamu wa afya.