News

Posted On:: Mar, 18 2021
News Images

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega amewapongeza viongozi na wananchi wa mkoa wa Kigoma kwa juhudi wanazofanya za kuibua, kulea na kukuza vipaji vya michezo na Sanaa katika wilaya zote za mkoa huo.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo mara baada ya kushiriki mbio za mwendo wa pole (jogging) pamoja na mazoezi ya viungo wakati wa fainali ya mashindano ya Kombe la “Nyumba ni Choo” kwa wilaya ya Kigoma Mjini yaliyoitimishwa Machi 16, 2021 katika uwanja wa Mwanga mjini Kigoma.

“Kigoma ni kitovu cha vipaji vya michezo na sanaa hapa nchini ni matumaini yangu msimu ujao Kigoma itakuwa na timu ya mpira wa miguu kwenye ligi kuu, nimefuatilia mchezo wa fainali kwa umakini na nimeona vipaji vingi vya hali ya juu kabisa, vijana wanajituma na wanacheza mpira wa kuvutia" alisema Naibu Waziri Ulega.