News

Posted On:: Dec, 28 2020
News Images

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega ameendelea kusisitiza umuhimu wa kurasimisha mchezo wa ngumi ili utambulike na kuheshimika.

Mhe. Ulega ameyasema hayo Desemba 26, 2020 Jijini Dar es Salaam alipohudhuria usiku wa Mapambano ya Ngumi ambapo amesema Serikali inatambua juhudi za wanamichezo wanaojituma kupitia nguvu zao na vipaji na itaendelea kuweka mazingira bora kwa sekta hiyo.

"Serikali tumejipanga vyema kutoa mchango kwa wapambanaji wetu, tunakaribisha wawekezaji na wadhamini wengi kudhamini mchezo huu ambao unatangaza vizuri Taifa letu" alisema Mhe.Ulega.

Mhe.Naibu Waziri Ulega ameongeza kuwa Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli anathamini sana vijana wapambanaji na dhamira yake ni kuendelea kukuza sekta hii ya Michezo,,Huku akieleza kuwa yeye pamoja na Waziri Mhe.Bashungwa watayasimamia vyema maono hayo.

Katika Mapambano hayo yaliyokua Mzunguko tofauti na ubingwa tofauti, watanzania Abdallah Pazi, Selemani Kidunda, Tony Rashid ,Ismail Gaitano na Mfaume Mfaume walifanya vizuri kwa kushinda Mikanda pamoja na Alama.