News

Posted On:: May, 04 2021
News Images

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewataka Wanahabari kufuata Miongozo inayozingatia hali bora ya kazi, ulinzi na usalama wa waandishi pamoja na uelewa wa matumizi ya Dijitali.

Waziri Bashungwa amesema hayo Mei 03, 2021 alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani inayofanyika Jijini Arusha.

Katika Maadhimisho hayo Mhe.Bashungwa ameeleza kuwa ni muhimu kwa Vyombo vya Habari kuwa na Mpango wa Maendeleo utakaowezesha vyombo hivyo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

"Serikali inahimiza wadau wote wa Habari,kuhakikisha wanaweka utaratibu unaowezesha kufanya ufuatiliaji na uwajibikaji katika kutekeleza Sera,na Sheria za taaluma hiyo" Mhe.Bashungwa.

Aidha Waziri Bashungwa ametoa wito kwa Viongozi kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Waandishi wa Habari pale inapohitajika kwa manufaa ya Umma na Maslahi ya Taifa letu kwa ujumla.

Maadhimisho hayo mwaka huu yanaongozwa na Kauli Mbiu "Habari kwa Manufaa ya Umma"