Habari

Imewekwa:: Dec, 02 2019
News Images

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ametangaza kuwachukulia hatua Wanamichezo wasiokuwa Wafanyakazimaarufu kwa jina la“Mamluki” wanaoshiriki Mashindano ya Michezo kwa Wafanyakaziinayojulikana kama SHIMUTAna SHIMIWI endapo watabainika.

Dkt.Mwakyembe amesema hayo leo Jijini Mwanza wakati akifungua michezo ya Mashirika ya Ummana Binafsimaarufu kwa jina la SHIMMUTA kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluh Hassan ambaye pia ndiye mlezi wa mashindano hayoambapo amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuimarisha afya za wafanyakazi,kubadilishana uzoefu pamoja na kutangaza Taasisi zao.

“Kuna hili suala la Wachezaji ambao sio wafanyakazi maarufu kwa jina la MAMLUKI kushiriki karika michezo hii,tena nakumbuka kuna kiongozi aliwahi kuwaita “viongeza nguvu bambikizi”,Hapa sio mahala pao nawataka wajiondoe mapema maana tukiwabaini wao pamoja na Taasisi zao tutawachukila hatua”alisema Waziri Mwakyembe

Mhe.Waziri Mwakyembe ameongeza kuwa wakati mwaka jana mashindano hayo yalipofanyika Jijini Dodoma Mhe.Makamu wa Rais Mama Samia hakuridhishwa na idadi ya washiriki kutokana na Idadi ya Makampuni na Mashirika yaliyopo nchini,hivyo kuagiza mkutano ufanyike kujua sababu na kuzipatia majibu ambapo maazimio yameleta matunda kwani mashindano ya mwaka huu idadi imeongezeka kutoka 26 hadi46.

Hata hivyo Mhe.Waziri amewataka waamuziwa mashindano hayo kuchezesha michezo hiyo kwa haki na kufuata sheria zote za michezona atakayesababisha vurugu au masononeko atawajibishwa kupitia kiapo alichoapa leo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bw.Khamis Mkanachi amesema kuwa Menejimenti za Taasisi za Umma pamoja na Makampuni binafsi zinatakiwa kuelewa kwamba wafanyakazi wao wanatakiwa kufanya michezo mbalimbali ili kuimarisha afya zao kwa ajili ya kuongeza ufanisi wanapokuwa kazini,hivyo ni wajibu wa kila Taasisi na mashirika kuona haja ya kutenga siku ya kufanya michezo.

“Michezo hii inafanyika kwa mwaka mara moja ni vyema viongozi wa Taasisi na Mashirika binafsi kuona umuhimu huo na kuwapa wafanyakazi wao muda wa kushiriki michezo hiyo inayoleta ari katika kufanya kazi” aliongeza Bw.Mkanachi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt.Fillis Nyimbi amesema Jiji la Mwanza hususan Wilaya ya nyamagana imeshukuru ujio wa mashindano hayo kwakua itaongeza kipato kwa wenyeji kutokana ongezeko la watu waliokuja kwa ajili ya mashindano hayo ambapo pia amewahakikishia amani na usalama.

Vilevile mwanamichezo Eliud Felix kutoka timu ya Jiji la Mwanza amesema michezo hiyo imewasaidia kujuana pamoja na kubadilishana uzoefu wa majukumu ya kila mmoja katika taasisi yake na kupendekeza iendelee kufanyika kila mwaka.

Mashindano hayo yalianza rasmi tarehe 27/11/2019 na yanatarajiwa kumalizika Desemba mosi 2019 ambapo jumla ya Mashirika na Taasisi 46 zimeshiriki ikiwemo wenyeji Ofisi ya Mkoa wa Mwanza,Chuo Kikuu Dodoma,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na nyingine.