Habari

Imewekwa:: Oct, 04 2019
News Images

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi amewataka Wafanyakazi wa Wizara hiyo kumpa ushirikiano Naibu Katibu Mkuu Dkt.Ally Possi ambaye aliteuwa na kuapishwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli hivi karibuni.

Bibi.Mlawi ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma katika kikao cha kumtambulisha Naibu Katibu Mkuu huyo kwa wafanyakazi ambaye ameripoti ofisi hivi karibuni baada ya kumalizika kwa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) lililokuwa likifanyika Jijini Dar es Salaam ambapo alishiriki baada ya kuapishwa wake.

‘Kama mlivyokuwa mkimpa ushirikiano Naibu Katibu Mkuu Bw.Nicholaus William aliyehama hivyo hivyo basi huyu mgeni nae mkampe ushirikiano vyema ili kuhakikisha majukumu ya wizara yanasonga mbele na tunafanikisha adhima ya serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi na kuleta maendeleo,’’alisema Bibi.Mlawi.

Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo aliendelea kufafanua kuwa kwa sasa ofisi za watumishi wa wizara zimegawanyika katika ofisi mbalimbali Dodoma kuna ambao wapo Mji wa Serikali Mtumba na wengine wapo katika Jengo la PSSSF na wengine wapo Dar es Salaam.

Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu huyo mpya Dkt.Ally Possi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo alisema anashukuru uongozi wa wizara hiyo kwa mapokezi mazuri na amesema yupo tayari kwa kujifunza masuala mapya ya kiutamaduni,Sanaa na Michezo.

‘’Nimefurahi kuungana na wizara hii ambayo inamajukumu ya kusimamia ustawi wa Utamaduni wa taifa letu pamoja na kusimamia Maendeleo ya Sekta ya Sanaa pamoja na Michezo,naahidi kuwapa ushirikiano katika masuala yote ya kikazi na milango ya ofisi yangu ipo wazi,’’Dkt.Possi.

Naye Mmoja wa Wafanyakazi hiyo Wizara hiyo Bibi.Lilian Lundo alitoa salamu kwa niaba ya wafanyakazi wenzake na kusisitiza kuwa watumishi wataendelea kumpa ushirikiano Naibu Katibu Mkuu huyo katika kutekeleza majukumu ya Wizara.

Halikadhalika kabla ya uteuzi huo Dkt.Possi alikuwa ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.