Habari

Imewekwa:: Jan, 03 2020
News Images

KaimuKatibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possiamewataka wafanyakaziwa Baraza la Kiswahili Taifa kuwa wabunifuwa miradi itakayoliletea taifa matokeo chanya katika kutangaza lugha ya Kiswahili kwenye nyanja za Kimataifa .

Dkt.Possi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaamalipotembeleaofisiza baraza hilo kwalengo kupata taarifa za utekelezaji wa mpango mkakati wake pamoja na kufahamu malengo ya taasisi hiyo katika kipindi cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

“Nawapongeza kwa mradi huu mzuri wa Kongoo sababu kazi mnayofanya yakuingiza maneno tabribani billion moja ya Kiswahili katika mtandaoitasaidiasana kukuza na kusambazalugha hii kwani sasa dunia imejikita zaidi katika tehama na shughuli nyingi zinafanyika kwa njia yamtandao hivyo uhifadhi wa maneno hayo ya Kiswahili katika mfumo huu ni hatua nzuri,”Dkt.Possi.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Kaimu Katibu Mkuu huyo aliendelea kusisitiza kuwa BAKITA ni taasisi muhimu kwa taifa na wizara ipo tayari kwa kuwawezesha kufanikiwa kutekeleza majukumu yake ya kuweza kufanikisha lughahiyo inasonga mbele sababu kukua kwa lugha hiyo ni ufahari kwaTanzania na haswa kama waasisi wa kutumia hugha hiyo.

Pamoja na hayo nae Katibu Mtendaji wa BAKITA Dkt.Selemani Sewangialitoa maombi Kaimu Katibu Mkuu huyo ya kuomba wizara iwasaidie katika kutangaza katika wizara mbalimbali kuwa wanauza Kamusi Kuu ya lugha ya Kiswahili iliyoandaliwa na baraza hilo yenye maneno mengikwaniuandaaji wa kamusi za Kiswahili ni moja ya majukumu yao.

“Tungependabaraza lianze kutoa mafunzo ya ukalimani kwa wahitimu wa chuo kikuu na wadau mbalimbali sababu tumeona kuna ombwe kubwala wataalamu wa lugha wanaoweza kufanya kazi ya ukalimani hivyo tungeomba kupatiwa fedha ili kuweza kufanikisha kununua vifaa vya kutoa mafunzo hayo,”alisema Dkt.Sewangi.

Halikadhalika Dkt.Sewangi aliwashukuruuongozi wa wizara kwa kuwapa ahadi ya kushughulikia suala ya baraza hilo kupata kiwanja cha kujenga ofisi ndani ya Jiji laDodoma ambapo ndiyo Makao Makuu ya Ofisi za Serikali .

Mbali na hayo nae mmoja wa wafakakazi wa baraza hilo ambaye ni Mfasiri Mkuu Bibi. Vidah Mutasaalitoa neno la shukrani baada kumalizika kwa kikao hicho cha kiongozi huyo wa wizara na wafanyakazi wa baraza kwa kuahidi kuchapa kazi na kuhakikisha wao kama mabalozi wa lugha hiyo wanahakikisha inasonga mbele.