Habari

Imewekwa:: Sep, 09 2019
News Images

Jamii imeshauriwa kutunza na kulinda dhana za jadi zinazotambulisha utamaduni ili kuendelea kuenzi na kukuza mila na desturiambazo ndio zinazotambulisha Taifa la Tanzania pamoja na kuwekakumbukumbu vizuri za jamii hizo.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Utamaduni wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Hadija Kisubi katika sherehe ya kusimikwa kwa Chifu wa Kabila la Wagogo Chifu Henry Mazengoiliyofanyika katika kijiji cha Mvumi Dodoma ambapo amesema kuwa jamii inapaswa kuhifadhi kumbukumbu zote za makabila yao kwakua ndio msingi wa utamaduni wa nchi.

“Taifa letu lina mila na desturi nzuri ambazo tunapaswa kuzilinda ,hivyo ni jukumu la kila jamii kuwa na makumbusho ambayo yatahifadhi mila na desturi lakini pia itasaidia kukuza utalii wa kiutamaduni”alisema Bibi.Hadija.

Ameongeza kuwa Serkali inatambua mchango wa Machifu na viongozi wote wa kimila katika kuelimisha jamii tamaduni ambazo ndio kioo cha Taifa letu hivyo jamii inapaswa kuzingatia ushauri na maelekezo yanayotolewa na Machifu hao.

Awali Mlezi wa Machifu Tanzania Mzee JohnMalecela amemshauri Chifu aliyesimikwa Mzee Henry Mazengo kufuata taratibu za kabila hilo katika uongozi wake pamoja na kuendelea kuhimiza watu wa jamii yake kulinda amani ya nchi.

Naye Chifu Mazengo ameahidi kulinda mila na desturi za kabila la wagogo ambazo zinaelekea kupotea kutokana na kabila hilo kuingiliana na makabila mengine lakini pia ameomba ushirikiano kwa ajimii yake ili kutimiza majukumu hayo vizuri.

Chifu Henry Mazengo amesimikwa kuwa Chifu wa pili Septemba 07,2019 kushika nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 baada ya Chifu wa kwanza wa kabila hilo Chifu Chaula Mazengo kufariki dunia.