News

Posted On:: Mar, 25 2021
News Images

Mnamo Machi 17, 2021 Taifa la Tanzania liligubikwa na Simanzi kubwa bada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (wakati huo akiwa Makamu wa Rais) alipotangaza msiba mkubwa wa aliyekua Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Taarifa hii iliwagusa watanzania na dunia kwa ujumla kutokana na mengi mazuri aliyoyafanya katika taifa hili.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ni Mionhoni mwa Wizara ambazo Dkt. Magufuli aliweka nguvu na mkazo mkubwa ili iweze kusaidia jamii kupitia sekta zake.

Dkt. Magufuli alikua mpenda michezo, Sanaa lakini pia alipenda Taifa lihabarike kupitia Sekta ya Habari kwa kutaka kila mwananchi apate habari zenye ukweli uhakika na kwa wakati sahihi kutoakan na utekelezaji wa Serikali kwa wananchi hao.

Marehemu Dkt. Magufuli Mwezi Februari mwaka huu alipozindua studi za Channeli Ten alitoa msisitizo kuhusu upatikanaji wa habari kuwa ni takwa la kisheria hivyo viongozi na wote wanaowajibika kutoa taarifa lazima wafanye hivyo.

Katika Sekta ya Michezo Dkt. Magufuli alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha Sekta hiyo inakua ambapo alisisitiza timu za taifa kufanya juhudi katika kutangaza nchi vizuri na hapa alisema “WATANZANIA TUNATAKA USHINDI TUMECHOKA KUSHINDWASHINDWA” ambapo katika uhai wake Timu ya Taifa ilifanikiwa kufuzu michuano ya AFCON kwa mara nyingine tangu baada ya miaka 30, timu za vijana Ngorongoro heroes pamoja na Serengeti Boys ziliitangaza nchi hii vizuri.

Mafanikio mengine katika sekta hii ni timu za wanawake za mpira wa miguu ya Twiga Stars ilifanikiwa kutwaa makombe mbalimbali, huku mchezo wa riadhana masumbwi nao ikiliheshimisha Taifa ndani na nchi, wakiwemo wanariadha Alphonce Simbu,Failuna Abdu na wanamasumbwi Hassan Mwakinyo, Dullah Mbabe na Mfaume Mfaume wakingara katika mchezo huo

Si hayo tuu Dkt. Magufuli aliwekeza katika miundombinu ya Michezo ikiwemo dhamira yake ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu jijini Dodoma, pamoja na marekebisho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Vilevile, Sekta ya Sanaa na Utamaduni ziliwahi kuongoza katika kuchangia katika pato la Taifa kati ya mwaka 2018 na 2019 kutokana na kuajiri vijana wengi ambao wanaendesha maisha yao kupitia sekta hizo.

Sekta hii pia itamkumbuka Dkt. Magufuli kwa maamuzi yake ya kuihamisha Taasisi ya Hakimili Tanzania (COSOTA) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Habari ilikua ni maamuzi ambayo yalikua yanalenga kusaidia sekta hii kwa karibu zaidi kulingana na wadau wake kuwa katika wizara hiyo.

Asante Dkt. Magufuliwizara ya Habari itakukukumbuka na itaendelea kukuenzi kwa kufanya kazi na kuwa karibu na wadau wake ili iweze kukidhi lengo la kuundwa kwake, ikiwemo kusimamia, Utamaduni wa nchi kwa kuendelea kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili kama alivyosisitiza enzi za uhai wake, kulinda na kuheshimu mila na desturi za nchi pamoja na muungano wetu.