Habari

Imewekwa:: Mar, 13 2020
News Images

Katika historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika,Tanzania ndiyo nchi iliyosimamia kupatikana kwa uhuru katika baadhi ya nchi za bara hilo.

‘Tanzania haitakuwa huru hadi nchi zote za Afrika zitakapokuwa huru” alisema Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hivyo aliungana na wanaharakati wenzake kama akina Samora Machel, Nelson Mandela, Kenneth Kaunda, Joaquim Chissano na wengine.

Hivyo katika kuenzi historia ya viongozi hawa namna walivyokomboa bara hilikutoka kwa wakoloni, mwaka 2003 wazo la utekelezaji wa programu hii lilibuniwa na Tanzania kwa kushirikiana na UNESCO lengo ikiwani kutambua na kuhifadhi kumbukumbu za harakati za kutafuta uhuru wa nchi za Afrika hasa nchi za Kusini mwa Afrika.

Tanzania ndiyo ilikuwa mwenyeji wa vikundi vingi vya wapigania uhuru ikiwemo kutoa hifadhi kwa Wapigania uhuru pamoja na kuweka Makao ya Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika ambayo yalikuwa Jijini Dar es Salaam ambayo yaliratibu harakati zote za ukombozi.

Mratibu wa Programu hii ya Ukombozi wa Bara la Afrika ambayo inaratibiwa na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Bi.Ingiahedi Mduma. Katika mahojiano na mwandishi wa makala haya alielezakuwaMwaka 2004 UNESCO iligharamia ujumbe wa Philip Mangula na wenzake ambao walikwenda Angola, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe kupata maoni ya wadau katika nchi hizo juu ya wazo hili.

Ujumbe huo ulipokelewa vema na nchi zote tano na ikapendekezwa kwamba mradi huo ujumuishe nchi zote za kusini mwa Afrika na utekelezaji wake usimamiwe na Tanzania ambayo inatambuliwa kuwa ni mdau mkubwa wa harakati hizo.

Ameeleza kuwa lengo la programu hii ni kuanzisha kituo cha Kikanda cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambacho kwa mujibu wa makubaliano kitajengwa Jijini Dar es Salaam, Tanzania, ambako Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika utatekelezewa, kuenziwa na kuoneshwa kwa ulimwengu.

Kituo hiki kitakuwa na Makumbusho, Maktaba, Nyaraka, Sehemu ya Watafiti na Ukumbi ambapo katika kituo hicho kutakuwa na uhifadhi kumbukumbu zote (picha, filamu, simulizi, barua, machapisho, maeneo yaliyotumiwa na wapigania uhuru, nyimbo, sare, ambapo Tanzania ndio iliyopewausimamizi wa zoezi hili .

Mwaka 2005 nchi 11 ziliungana na Tanzania kuwasilisha pendekezo la kuanzishwa kwa programu hiyokwa UNESCO ambapo nchi hizo ni Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lesotho, Mauritius, Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia, Swaziland, Zambia na Zimbabwe na baadae Mwezi Mei, 2010 Viongozi Wakuu wa vyama vya Siasa vilivyokuwa vya kupigania uhuru kusini mwa Afrika walikutana Jijini Dar es Salaam ili kuijadili Programu na hatimaye Mwezi Januari, 2011 Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika waliijadili Programu hii na kuipitisha.

Mwishoni mwa Mwaka 2019, Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza alifanya ziara kukagua namna maeneo ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika yanavyotunzwa, kuhifadhiwa na kuendelezwa katika kambi mbalimbali katika mikoa ya Dodoma wilaya ya Kongwa, Mororgororo wilaya ya Mvomero katika kambi ya Dakawa na Mazimbu Manispaa ya Morogoro pamoja na mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo.

Aidha, katika ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi alipokuwa anakaimu ofisi hiyo aliyofanya mapema mwaka huu aliagiza Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuhakikisha wanarasimisha Programu ya Urithi wa Ukomboziwa Bara la Afrika.

Dkt. Possi alitoa agizo hilo na kuitaka ofisi hiyo kuandaa Mpango Mkakati pamoja na Maandiko ya kuomba ufadhili wa program ambapo mpango huo utakuwa dira yanamna Programu itakavyotekelezwa sababuni ya kimataifa na siyo wa Tanzania pekee kwani kuna nchi za Afrika zinahusika na nchi za ulaya hivyo ni vyema kuwa na mpango madhubuti wa utekelezaji wa Programu hii.

Dkt. Possi alimtakaMratibu wa Programukuwa na Kanzi data ya Mawasiliano ya kila nchi iliyohusika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika kuanzia katika ngazi za Kitaifa mpaka Kimataifa na hii itarahisisha utekelezaji wa shughuli za programu na usambazaji wa taarifa.

Naye Mratibu wa Programu hiyo Bibi. Ingiahedi Mduma aliezeza changamoto za utekelezaji wa Programu hiyo na kusemakwa sasa kuna nchi ambazo tayari zimeonyesha nia ya kuchukua Programu hiyo ambazo ni Afrika Kusini Namibia na Angola, hivyo anaomba Serikali kusaidia kuwezesha mradi kwa kuwauna faida nyingi ikiwemo kuongeza ajira nafursa za utalii wa kihistoria.

Programu hii ilizinduliwa rasmi na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam tarehe 08 Desemba, 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Pamoja na hayo katika eneo la Mabwepande kumepatikana ekari 25 ambapo kitajengwa Kituo cha Kikanda cha Programu, na katika ukusanyaji wa taarifa kwa watu waliyoshiriki Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika wazee 227 wamehojiwa kutoka maeneo mbalimbali na yamehifadhiwa kwa nja ya kidijitali.

Vilevile Jumla ya Maeneo 255 yanayohusu programu hiyo yamebainishwa hapa nchini na yanaandaliwa utaratibu wa kukarabatiwa ili kuhifadhi historia iliyomo katika maeneo hayo,baadhi ni Mazimbu,Dakawa,Kongwa,Lindi Farm 17,Kihesa Mgagao etc, Pia picha 4000 kuhusu historia ya ukombozi wa bara la Afrika zimekusanywa nakuhifadhiwa na Mafaili 900 yenye nyaraka mbalimbali zinazohusu programu hiyoa yamepatikana na kuhifadhiwa.

Pia Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) wameiboresha Studio ya (external service) iliyotumika kurusha matangazo wakati wa harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika imekarabatiwa na kwa sasa imefanywa kuwa Makumbusho ya historia ya Ukombozi wa Afrika.

Ukarabati wa Jengo lililotumiwa na Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika unaendelea na jengo moja kwasasa ndiyo linatumiwa kama ofisi za Sekretarieti ya Programu.

Katika kuhakikisha programu hii inaendeshwa vyema serikali imeamua kuanzisha mchakato wa kutunga Sheria ya kusimamia na kuhifadhi maeneo yenye historia ya ukombozi unaendelea kutekelezwa.

Na nimatarajio ya serikali kuwa baada ya kufanya mapitio na kubaini mapungufu yaliyopo katika Mitaala ya Shule za Sekondari kuongeza mtaala wa historia ya Ukombozi wa Afrika na kuhakikishwainafundishwa kikamilifu katika shule za Sekondari hapa nchini na mapitio hayo yalifanywa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.