News

Posted On:: Jul, 18 2021
News Images

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefungua mbio za Kimataifa za Zanzibar zilizofanyika mjini Zanzibar Julai 18, 2021 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali, taasisi binafsi na wafanyabiashara.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi na Naibu wake, Dkt. Ally Possi pamoja na Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo Omary ni miongoni mwa wameshiriki mbio hizo ambazo zimeleta hamasa kubwa kwawananchi katika Visiwa hivyo pamoja na wananchi kwa ujumla nchini kushiriki kwenye mazoezi kwa lengo la kuimarisha afya zao hatua inayowapa nguvu ya kufanya shughuli za kimaendeleo.