News

Posted On:: Mar, 01 2021
News Images

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi Jumapili, Februari 28, 2021, amekagua mali mbalimbali za Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) zilizopo Dar es Salaam na kuagiza mali hizo ambazo zilitolewa kwa shirika hilo na viongozi wa awamu mbalimbali akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, zilindwe na ziendelezwe.

"Baadhi ya nyumba tangu mpewe hazina hati, baadhi ya viwanja havijaendelezwa lakini baadhi majengo mmeyatunza vyema, tuwaenzi viongozi waliokuwa na maono makubwa wakatupa mali hizo kusaidia Shirika kujiendesha, nawaagiza kwa kasi sasa mhakikishe mnaleta mawazo Serikalini kuendeleza viwanja mlivyo navyo lakini kampuni itumie fedha za ndani kukarabati baadhi ya majengo yake hasa la Mtaa wa Samora na nyumba iliyopo Upanga. Nitafuatilia tena, mkishindwa Wizara itavichukua kwa matumizi yaliyokusudiwa ambayo ninyi mnaonekana yanawashinda," alisema Dkt. Abbasi.