Kupata Kitambulisho cha Mwanahabari?

Maombi ya Kitambulisho cha Mwanahabari. Maombi lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo;-

•Barua ya Uthibitisho toka Chombo cha Habari husika au Taasisi ya Kielimu

•Nakala ya Vyeti vya Elimu vilivyothibitishwa pamoja na kitambulisho cha Mwanafunzi

•Picha tatu za paspoti. ADA: Muombaji anapaswa kulipia kiasi cha shilingi 30,000/=. Maombi ya Kitambulisho kwa Mwanahabari wa Nje ya Nchi. Maombi lazima yaambatane na vitu vifuatavyo;-

•Barua ya uthibitisho toka Chombo cha Habari husika •Nakala ya Paspoti ya Kusafiria

•Ushahidi wa Kitambulisho cha Mwanahabari toka nchi husika

•Picha tatu za paspoti ADA: Waandishi wa Habari toka nje ya nchi wanapaswa kulipia dola 500. Kuhusu masuala ya upigaji picha jongefu na kazi za makala, vibali zaidi vya uchukuaji filamu vitahitajika. Kutengeneza upya leseni ya Chombo cha habari. Maombi lazima yaambatanishwe na;- •Nakala ya leseni iliyokwisha muda wake

•Ripoti ya mwisho (idadi ya wafanyakazi, vyanzo vya fedha, namna biashara inavyofanyika n.k)

•Cheti cha ulipaji kodi •Makubaliano kuhusu usalama, afya/bima ya hatari. ADA: Gharama ya kutengeneza upya kwa leseni, mwombaji anapaswa kulipa shilingi 1,000,000/=