Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Kusajili Gazeti
Maombi ya Leseni ya usajili wa Gazeti/Jarida.
Maombi yanapaswa kuambatana na vielelezo vifuatavyo;-
- Cheti cha Usajili wa nyaraka yoyote ya kisheria.
- Barua kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu.
- Andiko la Mradi.
- Wasifu Binafsi wa Mhariri, waandishi na nakala ya vyeti vya taaluma ya habari.
- Nakala ya mwonekano (mpangilio) wa Gazeti/Jarida.
- ADA: Mwombaji anatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 1,000,000/=. kwa ajili ya kupata leseni.
Maombi ya Kitambulisho cha Mwanahabari. Maombi lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo
Barua ya Uthibitisho toka Chombo cha Habari husika au Taasisi ya Kielimu
Maombi ya Kitambulisho cha Mwanahabari wa kutoka Nje ya Nchi.
Maombi lazima yaambatane na vitu vifuatavyo;-
ADA: Waandishi wa Habari toka nje ya nchi wanapaswa kulipia Dola 500