Sera na Mipango

Idara hii inasimamia na kuratibu shughuli za Serikali ngazi ya Wizara. Katika kutekeleza majukumu yake, Idara imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Sehemu ya Sera, Sehemu ya Mipango na Bajeti na Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini. Majukumu ya Idara hii ni pamoja na;

•Kuratibu na kuandaa taarifa mbalimbali ambazo zinawasilishwa wizara ya Fedha pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu na maeneo mengine muhimu.

• Kuandaa na kuratibu uandaaji wa Sera mbalimbali za Wizara.

• Kukusanya na kuhifadhi takwimu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Wizara kwa ajili ya matumizi katika maamuzi ya Serikali.

• Kuratibu na kuandaa vikao vya kazi kwa ajili ya bajeti ya Wizara na Vikao vingine vya kisekta.