Majukumu ya Wizara

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ina majukumu yafuatayo:

Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera za Sekta za Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

  • Kuratibu na kusimamia masuala ya maendeleo ya vijana ili kuweza kujiajiri na kujitegemea.
  • Kuendeleza, kuwezesha na kuratibu masuala ya kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara.
  • Kusimamia Vyombo vya Habari (Magazeti na vituo vya Redio na Televisheni).
  • Kusimamia na kuratibu maendeleo ya michezo nchini.
  • Kusimamia na kuratibu maendeleo ya utamaduni nchini.
  • Kusimamia utendaji wa Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala, Miradi na programu zilizo chini ya Wizara.