Utawala na Rasilimali Watu

Idara hii inasimamia na kuratibu shughuli za utoaji wa huduma katika maeneo ya Utawala na Rasilimali Watu. Katika kutekeleza majukumu yake, Idara imegawanyika katika kutekeleza majukumu yake, Idara imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni Sehemu ya Utawala na Sehemu ya Rasilimali Watu. Majukumu ya Idara hii ni pamoja na;

• Kuratibu na kumshauri Katibu Mkuu kuhusu masuala yote ya kiutawala na utumishi;

• Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za utawala na utumishi;

• Kusimamia utekelezaji wa masuala ya utawala bora masuala mtambuka kama vile mazingira, vita dhidi ya rushwa ;

• Kusimamia masuala ya uhuaiano na maslahi ya wafanyakazi;

• Kusimamia masuala ya Usalama, Itifaki, Utunzaji wa kumbukumbu, Huduma kwa viongozi na shughuli za Bunge hasa zile za kiutawala na kiutumishi.