Utamaduni

Idara hii inasimamia na kuratibu shughuli zinazohusu utamaduni wa taifa letu. Katika kutekeleza majukumu yake, Idara imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Sehemu ya Mila na Desturi, Sehemu ya Sanaa na Sehemu ya Lugha. Majukumu ya Idara hii ni pamoja na;

• Kuimarisha na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania ambao ni utambulisho wa taifa letu.

• Kuhimiza na kukuza utaifa kwa vijana wetu na wananchi kwa ujumla.

• Kukuza Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa letu.

• Kufanya tafiti za lugha za asili za makabila mbalimbali nchini kwa lengo la kuziendeleza.