Habari

Waziri Dkt. Mwakyembe aunda Kamati ya Watu 10 kujadili sakata la TBC na Kampuni ya Star Times.

Imewekwa : 15th Jul 2017

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameunda kamati ya wajumbe 10 kwa ajili ya kufuatilia undani wa kutopatikana kwa faida kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kampuni ya Star Times kutoka China.

Soma zaidi

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AONGOZA WATANZANIA MECHI KATI YA GOR MAHIA NA EVERTON.

Imewekwa : 14th Jul 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan jana ameongoza Watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu ya Everton ya Uingereza na Gor Mahia kutoka Kenya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Soma zaidi

WIZARA YA HABARI YASHAURIWA KUONGOZA MABADILIKO YA UTAMADUNI WA KUTUMIA MUDA KIMKAKATI.

Imewekwa : 11th Jul 2017

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka amewataka watendaji wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa umma ya kuwa na utamaduni wa kutumia muda kimkakati ili kufanya kazi kwa bidii na kufikia malengo.

Soma zaidi

UTEUZI WA MWENYEKITI PAMOJA NA WAJUMBE BMT WASITISHWA.

Imewekwa : 11th Jul 2017

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.

Soma zaidi