Kusajili Gazeti

Maombi ya Leseni ya usajili wa Gazeti/Jarida. Maombi yanapaswa kuambatana na vielelezo vifuatavyo;- Cheti cha Usajili wa nyaraka yoyote ya kisheria. Barua kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu. Andiko la Mradi. Wasifu Binafsi wa Mhariri, waandishi na nakala ya vyeti vya taaluma ya habari Nakala ya mwonekano (mpangilio) wa gazeti/jarida. ADA: Mwombaji anatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 1,000,000/=. kwa ajili ya kupata leseni.